Kila mvuka mto hupima kwanza mkondo wa maji ili ajue kasi na nguvu ya maji kabla hajajitosa mzima mzima. Kisha hupima kina cha mto kabla ya kujiachia kilindini.
Vivyo hivyo msomaji hana budi kufahamu mada atakazokabiliana nazo katika darasa.Kwa mantiki hiyo,silabasi ni muhimu kwake,isije kuwa anaswagwa kama ng'ombe tu;aendako hakujui.
Mada za kiswahili kwa kidato cha tano na cha sita, kwa Kiswahili 1 ni:
•Ufahamu na Ufupisho.
•Matumizi ya Sarufi na Utumizi wa Lugha.
•Utungaji.
•Maendeleo ya Kiswahili.
•Tafsiri na Ukalimani.
Kwa kiswahili 2,mada zake ni:
•Fasihi kwa ujumla.
•Ushairi.
•Riwaya.
•Tamthiliya.
•Usanifu wa Maandishi.
Kila mada ina mada ndogo kadhaa ambazo nazo kila moja hudai muda wa kutosha kuikabili. Kwa mwanafunzi aliyeko shuleni, amepangiwa vipindi 10 kwa wiki vyenye dakika40 kila kimoja;hivyo ni muda wa saa 6 na dakika 40 (40×10 =400÷60=6.66...).
Ili mwanafunzi wa kujitegemea azisome mada vilivyo,hana budi kutenga muda wa takriban saa 1, kusoma kiswahili kila siku.
Kwa mpangilio huu, ataweza kusoma na kuzimaliza mada zote ndani ya miaka miwili.
Yote kwa yote, msomaji wa kujitegemea aweza kufanikiwa kwa kupangilia vizuri muda wake wa kusoma na kuutumia vilivyo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni